August 30, 2016

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

                                                          


                                            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuutaarifu Umma kuwa kupitia mradi wake wa uboreshaji wa miundombinu ya umeme ya Jiji la Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kutakuwa na uboreshwaji wa kituo kikubwa cha Kupooza na Kusambaza umeme Ilala, cha Msongo wa Kilovolti 132 Ubungo - Ilala. Kuanzia siku ya  tarehe: 03 Septemba mpaka tarehe 25 Septemba, 2016. Katika kipindi hicho kituo cha Ilala kitakuwa kinazimwa ili kufanya maboresho.

Sababu za uboreshwaji wa miundombinu ya umeme kwa Jiji la Dar Es Salaam
·         Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora  kwa kumruhusu Mkandarasi (TAKAOKA) kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka zenye uwezo mkubwa za laini mbili za msongo wa kilovolti 132.
·         Kuboresha vituo vya kupooza na kusambaza umeme vya Ubungo na Ilala kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi .
·         Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye laini mbili za Ubungo - Ilala.
Wakati wa uboreshaji huu wateja wetu wataathirika kwa tarehe  03, 04, 10, 11, 17, 18, 24 na 25 Septemba, 2016, muda ni kuanzia saa 02 asubuhi hadi saa 11 jioni.

MAENEO YAFUATAYO YATAATHIRIKA:
Maeneo yote ya kati kati ya jiji, Maeneo yote ya Upanga, Maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Mbagala yote, Chang’ombe yote, Kiwanda cha Saruji Maweni, Wizara ya Utalii, Tusiime Mission, Tanzania Oxygen, Ofisi ya Manispaa ya Temeke, Unilever, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana Printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya afya, Bandari geti na maeneo ya jirani.

Maboresho haya ya miundombinu ya umeme yanalenga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana katika jiji la Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment