August 15, 2016

KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI TAREHE: Jumatano 17 Agosti, 2016, TAREHE: Jumatano 17 Agosti, 2016


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

1.LAINI YA KUNDUCHI
TAREHE: Jumatano 17 Agosti, 2016.
MUDA: 3:00 Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya KUNDUCHI, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya Mbezi beach, Mbezi juu, Interchick, Kobil na Camel petrol station, Agape TV, Kwa Maranda, ST.Marys, Baraza la mitihani, Kiwanda cha Kilai pamoja na maeneo ya jirani.

2.LAINI YA MASAKI (MS3)
TAREHE: Jumatano 17 Agosti, 2016
MUDA: 3:00 Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya Masaki (MS3), kwa ajili ya kuhamisha laini ya msongo 11KV ya umeme na kupisha ujenzi wa laini mpya ya msongo 33KV ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya maeneo ya Oysterbay, Masaki, Masaki Chole road, Valahala, Msasani, UN, Mzingaway, Double tree, Kipepeo, pamoja na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 / 0768 985 100

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na : OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.

2 comments:

  1. Nashukuru Kwa taarifa Kama Hizo huko DAR lakini Sisi huku Kwetu Rufiji mnatukati Huo umeme bila kutoa taarifa sasa-sijui huku Hakuna umuhimu wa kutoa taarifa AU HII songasi hausiani Rangi kidato Maana mnakata Kama kibatari kimepata Zaruba ya Upepo wa kimbunga cha gafla to kutwa mnatukatia to Siku Zaidi ya Mara 7-10 Hii Ni Haki AU sharia IPO DAR huku Kwetu Rufiji Hakuna Jibu

    ReplyDelete
  2. Nashukuru Kwa taarifa Kama Hizo huko DAR lakini Sisi huku Kwetu Rufiji mnatukati Huo umeme bila kutoa taarifa sasa-sijui huku Hakuna umuhimu wa kutoa taarifa AU HII songasi hausiani Rangi kidato Maana mnakata Kama kibatari kimepata Zaruba ya Upepo wa kimbunga cha gafla to kutwa mnatukatia to Siku Zaidi ya Mara 7-10 Hii Ni Haki AU sharia IPO DAR huku Kwetu Rufiji Hakuna Jibu

    ReplyDelete