September 22, 2014

KUOMBA RADHIShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaomba radhi wateja wake wote wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Shinyanga, Mwanza na Manyara kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti siku ya Jumapili na Jumatatu Septemba 21 na 22, 2014.
SABABU za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo katika mikoa hiyo, ilikuwa ni hitilafu kwenye mashine mbili za kufua umeme katika Kituo cha Pangani na hitilafu kenye njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 132 kutoka Chalinze hadi Hale.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment