September 9, 2014

TAARIFA KWA UMMA 
Bw. TOM  MWAISUPULE

UONGOZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), unapenda kuutaarifu umma kuwa Bw. Tom Mwaisupule (pichani juu) aliyekuwa mwajiriwa wake Mkoa wa Temeke kama Fundi Umeme (Linesman), si mwajiriwa tena wa TANESCO kuanzia Agosti 19, 2014.
Kwa sababu hiyo,  Shirika linatoa tahadhari kuwa halitahusika na kazi au makubaliano yoyote yatakayofanywa na Bw. Tom Mwaisupule  kwa niaba ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Imetolewa na:      Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO - Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment