September 5, 2014

TANGAZO LA KATIZO LA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA KILIMANJARO NA ARUSHAShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kuwa, kesho Jumapili Septemba 07, 2014 kutakuwa na katizo la umeme kwa baadhi ya maeneo katika mikoa hiyo kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

SABABU:                  kupisha matengenezo makubwa na ya lazima kwenye kituo cha kusambaza umeme cha Hale cha msongo wa kilovolti 132.


Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo  0784/0715-271461, Kituo cha miito 2194400 AU0768- 985100.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment