September 2, 2014

TAARIFA KWA UMMA



UONGOZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), unapenda kuutaarifu umma kuwa Bw. Sylvester Alphonce Mashauri (pichani juu) aliyekuwa mwajiriwa wake mkoa wa Tanga kama Fundi Umeme, si mwajiriwa tena wa TANESCO kuanzia Septemba 1, 2014.

Kwa sababu hiyo, Shirika linatoa tahadhari kuwa halitahusika na kazi au makubaliano yoyote yatakayofanywa na Bw. Sylvester Mashauri kwa niaba ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


Imetolewa na:      Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO - Makao Makuu.
 


No comments:

Post a Comment