September 16, 2014

TAARIFA KWA UMMA

                                   
                                       KIZITO STANSLAUS MAYUNGA

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautangazia umma kuwa mtajwa hapo aliyekuwa Mhasibu Wilaya ya RUANGWA, si mfanyakazi tena wa (TANESCO) kuanzia Mei 27, 2014.

Kwa sababu hiyo, Shirika halitahusika na kazi au makubaliano yoyote yatakayofanywa na Bw. Mayunga kwa niaba ya TANESCO.

Aidha Bw. Kizito anatafutwa na mwajiri wake popote alipo. Kwa yeyote atakaye muona atoe taarifa Ofisi zozote za TANESCO au Kituo chochote cha Polisi kilicho karibu. Zawadi nono itatolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwake. Shirika limemfungulia jalada polisi kwa RB RUN/RB/1261/2014 na RUN/IR/877/2014.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment