September 11, 2014

TAARIFA KWA WATEJA WETU WA TEGETA CHANIKA - BOKO DECA INN

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linawataarifu wanateja wake wa maeneo ya Tegeta Chanika, Tegeta Nyaishozi, Tegeta Masaiti, Boko, Bunju, Ununio, Mbweni, Mabwepande, Burumawe na Boko Deca Inn, Kutakuwa na kuzimikazimika kwa umeme kutokana na mamlaka ya maji kutandaza miundo mbinu ya maji (mabomba) pembezoni mwa barabara hivyo TANESCO kulazimika kuhamisha laini ya umeme Tegeta- Chanika mpaka Boko Deca Inn.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakao kuwa unajitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
Tanesco Makao Makuu.

2 comments:

  1. Nashindwa kuelewa, kwani dawasco waliamua leo kutandaza hayo mabomba? Zero communication between shirika zetu,

    ReplyDelete