September 1, 2014

TAARIFA KWA UMMA

    Kutokana na tatizo lilitokea usiku wa kuamkia jumamosi tarehe 30 agosti 2014 la kukatika kwa umeme na kuathiri maeneo ya Kisarawe,Gongo la Mboto,Kivule,Kipuguni,Ukonga,Tabata,Uwanja wa ndege,viwanda vilivyopo barabara ya nyerere,Chang'ombe na Tandika,shirika la umeme nchini-TANESCO linapenda kuwajulisha kuwa tatizo hilo lilitokea kwenye Kituo cha umeme cha Kipawa ambapo Transformer kubwa ya MVA 90 au MW 90 ilipata hitilafu na isingeweza kuwashwa.
    Kutokana na tatizo hilo wateja wa maeneo hayo yote waliunganishiwa umeme kupitia njia ya umeme ya kutoka Ubungo ambapo hadi jumapili wateja wote wa majumbani walirejeshewa umeme isipokuwa wateja wakubwa wa viwandani.
    Jitihada zinazoendelea kufanyika kwa sasa ni kufungwa Transformer nyingine ambayo inauwezo huo huo wa MW 90 na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika siku ya jumatano ili umeme urejee katika hali ya kawaida.wakati huo huo mafundi wa shirika wakisaidiana na mtaalam kutoka India wameanza kutoa mapipa ya mafuta 300 ili kuichunguza zaidi transformer hiyo iliyoharibika.
 
 Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
    

No comments:

Post a Comment