August 22, 2014

KUANZA KWA OPERESHENI KABAMBE YA KUKUSANYA MADENI YA UMEMEKUANZIA SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU, SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) LITAANZISHA OPERESHENI KABAMBE NA ENDELEVU YA KUKUSANYA MADENI YA WADAIWA WAKE WOTE KWA NCHI NZIMA.

UONGOZI WA SHIRIKA UNATOA MUDA WA SIKU 10 HADI AGOSTI 31, 2014 KWA WATEJA WAKE WOTE BINAFSI NA TAASISI ZOTE ZA SERIKALI AMBAO HAWAJALIPIA ANKARA ZAO ZA UMEME KWENDA KULIPIA HARAKA IWEZEKANAVYO. BAADA YA MUDA HUO KWISHA, HUDUMA YA UMEME ITASITISHWA BILA TAARIFA ZAIDI.

OFISI ZA TANESCO ZITAKUWA WAZI SIKU ZA JUMAMOSI NA JUMAPILI ZA TAREHE 23, 24, 30 NA 31 ILI KUTOA NAFASI ZAIDI KWA WADAIWA WOTE KULIPIA ANKARA ZAO.

UONGOZI UNASISITIZA KUWA ZOEZI HILI LINAHUSU WATEJA WAKE WOTE, WATU BINAFSI NA TAASISI ZA SERIKALI.

KUEPUKA USUMBUFU, KALIPIE BILI YAKO SASA.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI,
TANESCO MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment