August 2, 2014

TAARIFA KWA UMMA

BW. DEONATUS M. KIHEKA

Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautangazia umma kuwa mtajwa hapo aliyekuwa Mhasibu Kituo cha Ngara Mkoa wa Kagera si mfanyakazi tena wa (TANESCO) kuanzia Juni 10, 2014 kutokana na yeye mwenyewe kujiachisha kazi kutokana na utoro bila taarifa yeyote kwa mwajiri wake (Absconded).

Kwa sababu hiyo, Shirika halitahusika na kazi au makubaliano yoyote yatakayofanywa na Bw. Kiheka kwa niaba ya TANESCO. 


Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.


No comments:

Post a Comment