August 1, 2014

MKOA WA KINONDONI KUSINI

                                  KATIZO LA UMEME MKOA WA KINONDONI KUSINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 02/08/2014 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi 11:00 Jioni.  Sababu ni Matengenezo makubwa kwenye mitambo ya kupoza na kusambaza umeme iliyoko Ubungo.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo yote ya Magomeni, Ubungo, Tandale, Sinza, Kimara , Mbezi,  Kibamba, Mabibo, Kigogo, Changanyikeni, Makongo, Chuo Kikuu cha DSM, Survey,  Mabibo hostel,  Chuo Kikuu cha Ardhi na maeneo yote jirani na hayo.

Tafadhali: Usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo 0784271461, 0715271461,  Au Call centre number 2194400 or 0768 985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na :         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.


No comments:

Post a Comment