September 11, 2013

DODOMA

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA DODOMA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa mkoa wa Dodoma kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI 14/09/2013 kuanzia Saa 03:00 asubuhi - 12:00 jioni.  Sababu ni kubadilisha nguzo zilizochakaa na kufunga “braker”.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
Wilaya ya Kondoa – Aya Sekondari, Mondo, Kelema Maziwa, Dalai, Jenjeluse, Goima, Songolo, Hamai, Churuku na maeneo ya jirani.
Wilaya ya Kiteto – Maeneo yote ya Kiteto, Chamanda, Mlijo juu, Mrijo Chini, Soya, Mapango, Matui, Dosidosi, Enguselo, Njoro, Chekanao, Kipelesa, Kiteto Mjini na maeneo ya jirani.
TAFADHALI USIGUSE WALA KUKANYAGA NYAYA ZILIZOANGUKA, toa taarifa kupitia namba zifuatazo: 026 2321728, 0732961270, and 0732961274. au namba za huduma kwa wateja 2194400 or 0768 985 100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:     OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment