September 12, 2013

KILIMANJARO

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA

KATIZO LA UMEME –MKOA WA KILIMANJARO

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)  linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kilimanjaro wa Wilaya  Same kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya Jumamosi September 14, 2013 kuanzia Saa 03:00 hadi Saa 10:00 Jioni.  Sababu ni kubadilisha nguzo zilizooza katika laini kubwa ya umeme ya Makanya.
ENEO LITAKALO ATHIRIKA NI:-
Vudee, Makanya, Hedaru, Suji, Chome, pamoja na Tae
‘‘usiguse wala kusogelea waya uliokatika au kuanguka chini,  toa taarifa kwenye ofisi ya TANESCO kupitia namba 0272755007 ,0272755008, na 0682771310, 0765397925
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
IMETOLEWA NA:  OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment