Siku ya Jumanne tarehe
17-09-2013 Mkoa wa Temeke ulimkamata KISHOKA
aliyejitambulisha kwa jina la Benard Kilembe mkazi wa Yombo
Vituka. Kishoka huyu alieleza kuwa aliwahi kuwa mfanyakazi wa muda maalum Tanesco-Mbeya
miaka ya 1995-1997.
Baada ya kupekuliwa nyumbani
kwake, alikutwa na nyaraka mbalimbali za shirika kinyume na
taratibu, sare ya Ijumaa(T shirt) na Shati la Sare za
mafundi, Rakili mali za Shirika
(seal), vipande vya nyaya 50mm na 25mm,kitambulisho
cha aliye kwenye mafunzo na
na pamoja na hayo alikuwa amejiunganishia umeme kinyume cha taratibu.
Kishoka huyu bado yupo chini ya ulinzi kwenye kituo cha polisi Chang’ombe akiisaidia polisi na uchunguzi zaidi.
Akiwa chini ya ulinzi
Daftari la wateja anaowatembelea
Kitambulisho anachotumia kufanya shuguli zake
No comments:
Post a Comment