September 25, 2013

MKOA WA PWANI WILAYA YA KISARAWE

TAARIFA KWA UMA
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kisarawe  kumekuwa na tatizo la kukatika katika kwa umeme  maeneo ya mwisho wa Lami,Pugu,Majohe,Chanika,Buyuni na Kisarawe tokea siku ya Ijumaa tarehe 20/09/2013.
Hali hii imesababishwa na watu wasiowema kukata na kuchoma nguzo za laini kubwa hivyo kusababisha kukatika katika kwa umeme nakupelekea baadhi ya vifaa vinavyothibiti mwenendo wa umeme kwenye kituo chetu cha kupozea umeme kilicho Gongo la Mboto kupata hitilafu.Mafundi wetu wamesharekebisha tatizo hili na sasa hali itarejea kama kawaida pamoja na marekebisho madogo madogo yatakuwa yakifanyika pindi yatakapojitokeza.
Tunaomba radhi kwa tatizo hili ambalo lilikuwa nje ya uwezo wetu.Pia tunawaomba wananchi wasiowema kuacha vitendo vya kuhujumu miundo mbinu ya umeme kwa kuwa inalisababishia shirika hasara kubwa na kusababisha usumbufu kwa wateja wetu.
Imetolewa Na:-      Ofisi ya Uhusiano
                                Tanesco-Makao Makuu            
                         

7 comments:

 1. Na eneo letu ni pugu kajiungeni umeme wetu unakero unazima unawaka unazima unawaka manaake nini au mpaka ulete shoti uuwe watu hizo mita mpya kazitupeni jalalani

  ReplyDelete
 2. Na eneo letu ni pugu kajiungeni umeme wetu unakero unazima unawaka unazima unawaka manaake nini au mpaka ulete shoti uuwe watu hizo mita mpya kazitupeni jalalani

  ReplyDelete
 3. Watu wa mtaa wa mwalampuka gogo kimwani, hatuna umeme mpaka sasa na jitihada zetu zimegonga Mwamba baada ya kuambiwa kugharamia mradi sisi wenyewe wananchi maskini wenye vipato vidogo, inawezekana sio sehemu sahihi hapa nilipoandika lakini tambueni na sisi ni wananchi na tunachangia pato la serikali kwa kukatwa kodi sasa kwa nini umeme tunausikia kwa majirani na vijiji vingine vya mikoani na sisi tupo tu, maswala yote yashafikishwa kwa mkurugenzi wa tanesco kisarawe jibu lake tujigharamie wenyewe mradi ambao kimahesabu hatuwezi zaidi ya kusubiria miujiza, wakazi wapo zaidi ya kaya 300 na majina ya baadhi ya wanajamii yashawafikieni, chonde chonde nawaomba mfanye jambo katika hili

  ReplyDelete
 4. Tanesco kisarawe huduma ipo kwa mtu binafsi wala si ofisini.
  tuna uliza ofisi ya kutoa huduma kulinga na utaratibu ipo wapi?
  kama ni mkoani au wizarani tuelekezwe ili tufuate huduma huko.Njia nyingine hatuziwezi kabisa nafikiri naeleweka vizuri.
  hatujui utaratibu ukoje wa umeme?hatuwezi kulipia mpaka mwenye hiyo ofisi ya kupima aamue na meneja sijui anatueleza nini?

  ReplyDelete
 5. Tanesco Kisarawe Tanesco kisarawe kweli kila kitu kinahitaji nani aje waziri,takukuru,tamisemi,rea,wizara, mkurugenzi,mkuu wa mkoa aje kuwahimiza ?????
  Mi nafikiri Takukuru taifa wakaweke kambi pale ofisi ya Tanesco kisarawe ili waweze kuhudumia wateja wote waliokwisha lipa wapatiwe huduma kuliko kukaa na hela zetu bila huduma..nendeni benki mtaina jinsi wanachi wanavyolipa lakini hakuna huduma sasa kwanini...?
  Tanesco makao makuu tunaomba muwapunguzie eneo la kufanyia kazi tanesco kisarawe la sivyo wananchi tuna umia sana na hatuna hata za kutoa pembeni ili tupate huduma......
  nani anaweza kutuisaidia ? waziri? mkuu wa mkoa? nani yupo karibu na huduma kwa wananchi? tunauliza tamisemi?

  pale kuna magenge ya kufanya mipango nani,wapi na lini? umeme upelekwe? tumechokaaaaa na huduma mbovu toka ofisi ya tanesco kisarawe ...tufanye nini tunafuata utaratibu hakuna huduma kabisa ....tuko nchi gani ?
  ni bora eneo la ilala lihudumiwe na ofisi iliyokaribu kuliko kisarawe.....Tanesco kisarawe ni aibuuu sanaaaa!

  ReplyDelete
 6. Kwa Kweli Tanesco Kisarawe Mnaliaibisha sana Shirika hili kubwa la Tanesco...!Naomba Siku mpate ugeni wa dharura hapo kwenu; ndipo mtakapojua kwa nini barabara ya mwendokasi haina bumps...

  ReplyDelete
 7. YAAAAAANI TANESCO TANZANIA AKUNA KAZI MNAYOFANYA KAZI YENU KUONEA WATU NA KUWALIA ELAZAO...NAONGEA HIVI KWA MACHUNGU SANA BAADA YA KULIPIA MITA MPYA NA BAADA YA MWEZI MMOJA MITA IKAANZA KUSUMBUA ALAFU KILA NIKIPIGA WANANITUMIA NAMBA YA KU RESET NA UMEME UNARUDI...MWISHO WA SIKU WAKAANZA KUSEMA ETI KWANGU KWAKUA KUNA SALON NDO MAANA UNAKAA UNAKATA KWAIYO NINUNUE STABILIZER ..NDO NIKAAMUA KUFUNGA SALON YANGU NA BADO BAADAE UKAENDELEA KUKATIKA NA PIA NASHANGAA NIKIWADAI WAJE WANIBADILISHIE MITA MPYA WANADAI ETI NIKALIPIE TENA LAKI MBILI NA NUSU...HIVI AKILI ZENU ZINAFANYA KAZI KWELI??????MI NAENDA SEHEMU NAKUTA ELA TU IPO YA KUCHEZEA???KWAIYO MNABAMBIKA WATU MITA MBOVU ILI WALIPIE TENA ???MIMI ILI SWALA LANGU LITAFIKA IKULU KWA MR PRESIDENT...NA MTU AMBAYE AMEKUA AKINAMBIA NIMPE ELA HAPO KWENU ATALIJUA JIJI MANAKE WANASEMA KWA LAKI NA NUSU FASTA UNAPATA MITA NA UNAFUNGIWA SIKU HIYO HIYO...KWAKELI INANIUMA MPAKA KUMOYO...BIASHARA ZANGU ZIMEKUA MBOVU KISA NYIE TANESCO...NAAKIKISHA NAONDOKA NA MTU HAPO

  ReplyDelete