September 19, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA MWANZA.



Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwataarifu wateja wake wa mkoa wa Mwanza, kuwa kutakuwepo na katizo la umeme kama ifuatavyo:


SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 21/09/2013, kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 8.00 mchana.Maeneo yatakayoathirika ni NYASAKA, BUZURUGA, MWANANCHI, BUSWELU, KANGAE, MWATEX.NYAKATO STEEL NA MECCO.

SABABU YA KATIZO HILI NI MATENGENEZO KATIKA KITUO KIPYA CHA KUPOOZEA UMEME CHA NYASAKA.

TAHADHARI

Wateja wa maeneo tajwa  hapo juu wanaombwa wazime vifaa vyote vinavyotumia umeme kwa muda huo wa matengenezo hayo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza , Tafadhali usishike,usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini ,unaweza kuwasiliana  na kitengo  cha  dharura TANESCO Mwanza  kupitia namba 028 250 0090 , 028 250 1060.

SHIRIKA LINAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA. 
                       
 Imetolewa na:

                                Ofisi ya Uhusiano.
                              Makao Makuu.        

No comments:

Post a Comment