Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwaarifu wateja
wake wa Mkoa wa Morogoro kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-
TAREHE: Jumapili Septemba 15,
2013
MUDA: Saa 3:00asubuhi
hadi Saa 12:00jioni
SABABU: -
Kufanya matengenezo ya tahadhari
kwenye Transfoma namba 1 ya Msongo Mkubwa wa kilovolti 220, 132 na 33 ili
kuzuia mafuta yanayovuja na kufanya marekebisho makubwa kwenye switchi ya
msongo wa kilovolti 33.
NIA:-
Kuzuia katizo la ghafla la umeme
linaloweza kutokea wakati wowote na kusababisha uharibifu wa vifaa vya umeme
kwenye mfumo.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
Maeneo yatakayoathirika ni Mkoa wote wa Morogoro
Tafadhali usishike au kukanyaga waya wowote
uliodondoka, Toa taarifa Ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu nawe au tupigie
simu ya Kituo cha Miito na Huduma kwa Wateja namba 2194400 au 0768 985100
IMETOLEWA NA: OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment