Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mikoa ya Ilala na Temeke kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-
MKOA WA ILALA:
TAREHE: 12/10/2013; Jumamosi
SAA: 3:00 Asubuhi - 11:00 Jioni
SABABU: Kubadilisha
Nguzo Zilizooza, kufanya Matengenezo na Kukata matawi ya Miti Katika Njia ya Umeme ya Msongo mkubwa wa Umeme wa R2 na R3
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Makao
Makuu ya Polisi-Central, Ofisi za TRA-Long Room, Bandari, Jengo la
Water front, Shoprite Supermarket Kamata na maeneo ya jirani,
Ofisi za Tigo Makao Makuu Mtaa wa Lugoda na maeneo ya jirani, maeneo
yaliyoko mtaa wa Makamba, maeneo yaliyoko pembezoni mwa barabara ya
Shule ya Uhuru, maeneo yaliyoko Mtaa wa Muheza, Baadhi ya Maeneo ya
Clock Tower, na maeneomachache ya Mnazi Mmoja.
MKOA WA TEMEKE:
TAREHE:
Jumamosi 12/10/2013,
MUDA: Saa 3
Asubuhi - 12 jioni
SABABU:
Kufanya ukarabati kwenye kituo kikubwa cha umeme chenye msongo wa
kilovolt 33/11kv cha Tandika na kukata miti
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Yombo yote na baadhi ya maeneo ya Tandika.
Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa upesi kupitia simu zifuatazo: Mkoa wa Ilala 022 213 3330, 0784 768586,
Mkoa wa Temeke 2138352; 0712052720; 0758880155 au namba hii ya kituo cha huduma kwa Wateja 2194400 au 0786985100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment