KUOMBA RADHI
Shirika la Umeme Tanzania
TANESCO
linaomba radhi wateja wake wa Bagamoyo kwa katizo la umeme lililotokea
kuanzia siku ya Jumapili Oktoba 6, 2013 saa 7:30 mchana hadi Jumatano
Oktoba 9, 2013 saa 5:25 usiku kutokana na kuharibika kwa transfoma
kubwa la MVA 2.5 ya msongo wa kilovoti 33/11 iliyopo
Mwanamakuka.
Transfoma mbovu imeondolewa na kuwekwa nyingine ya MVA 7.5 na umeme sasa unapatika wa kutosha.
Shirika linasikitika sana kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi chote cha tatizo hili.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment