October 4, 2013

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI 05/10/2013 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi hadi Saa 5:00 Asubuhi.  Sababu ni kubadilisha nguzo zilizooza katika line ya Msongo wa 33kV.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Mkuranga, Vikindu na Kisemvule

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 023 2440061, 0657 108782 au Kituo Cha Kupokea Miito ya Simu namba 2194400 au 0768 985 100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.


No comments:

Post a Comment