October 3, 2013

MWANZA

KATIZO LA UMEME MKOA WA MWANZA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Mwanza kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 05/10/2013 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi saa 6:00 Mchana.  Sababu ni matengenezo kwenye kituo kikubwa cha kusambazia umeme cha 220/132/33Kv kilichopo Nyakato.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Nyakato steel, Nile perch, Serengeti Breweries, Pepsi, Igoma na Kisesa.
TAHADHARI
Tafadhali usishike, usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini, toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:- 028 250 0090 , 028 250 1060.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
                  
Imetolewa na:       OFISI YA UHUSIANO.
MAKAO MAKUU.                                                                  

No comments:

Post a Comment