October 9, 2013

DODOMA

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA DODOMA
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa mkoa wa Dodoma kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya IJUMAA tarehe 11/10/2013 kuanzia saa 3:00 Asubuhi hadi 11:00 Jioni.  Sababu ni kubadilisha nguzo zilizochakaa.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Hospitali ya Ntyuka DCMC, Kiwanda cha Maji ‘’AHSANTE’’ Chuo Kikuu Dodoma, Maeneo ya Kisasa, Nzuguni, Nane nane, Ihumwa Jeshini (JWTZ), Ihumwa Kijijini, Kijiji cha Hombolo, Mtumba, Vikonje, Chamwino Ikulu, Buigiri, Chinangali I, Chalinze, Chilonwa, Manchali, Maeneo yote  ya Wilaya ya Chamwino, Kongwa, Gairo na Wilaya ya Mpwapwa.
TAFADHALI USIGUSE WALA KUKANYAGA NYAYA ZILIZOANGUKA, toa taarifa kupitia namba zifuatazo 026 2321728, and 0732961274. au Namba za huduma kwa wateja 2194400 or 0768 985 100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:     OFISI YA UHUSIANO.
        TANESCO – MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment